Header

Kelvin Yondani aiponda Simba Sc

Beki kisiki na tegemeo wa Mabingwa watetezi Yanga, Kelvin Yondani ameitupia kijembe timu yake ya zamani ya Simba, kwa kutamka kuwa hajutii kutua Jangwani kutokana na mataji mengi ya ubingwa wanayoyachukua tangu asaini kukipiga timu hiyo.

Kauli hiyo, ameitoa mara baada ya kumalizika mchezo dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa jijini Dar juzi Jumamosi ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

“Hivyo, hata sijutii kuondoka Simba na kuja huku Yanga nikiendelea kubeba makombe ya ligi kuu na nikuhakikishie nitaendelea kubeba makombe hadi nitakapoondoka Yanga,” alisema Yandani.

Yondani ambaye aliamua kuondoka Simba baada ya Yanga kueka dau kubwa ambalo alikuwa akiliitaji na akusita kufanya hivyo kwani alichokuwa akiitaji Yanga walitimiza.

Comments

comments

You may also like ...