Header

Kocha Mwambusi awapiga Mkwara mzito Toto Africa

Kocha msaidizi wa Yanga SC Juma Mwambusi ameizungumzia mechi yao ya kesho dhidi ya Toto Africa kama mechi ngumu na yenye ushindani mkubwa.

Akiongea na waandishi wa habari leo Asubuhi ametanabaisha kuwa  benchi la ufundi wameiandaa vyema timu yao kucheza kwa ushindani ili washinde mechi hiyo na kujiweka katika mazingira mazuri ya kubeba ubingwa wa ligi kuu.

” tunatambua Toto kesho watacheza kwa tahadhari kubwa ili kupata ushindi lakini tumewaandaa vyema wachezaji kimbinu, kiufundi na kisaikolojia ili kushinda uchovu na kucheza kwa moyo wote ” Alisema Mwambusi

Mwambusi akuishi hapo na  kusema anafahamu Toto Africa watakuja kwa mchezo wa kukamia hata kuwashangaza wengi kwanini wanapambana sasa wasishuke daraja lakini wao kama Yanga SC wanalifahamu hilo na wanazoefu nalo kama ilivyokuwa katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Mbeya City.

Yanga SC watacheza na Toto Africa kesho uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni ikiwa ni mechi yao ya 29 kuelekea mwishoni mwa msimu na alama zao 65 kileleni mwa ligi

Comments

comments

You may also like ...