Header

P-Funk akiri kuwa ni Darassa ndiye aliyempa hamasa ya kuja na muziki tofauti

Hata wakongwe hupata inspiration kutoka kwa wadogo zao na hicho ndicho kilichotokea kwa producer nguli wa Bongo Flava, P-Funk Majani.

CEO huyo wa Bongo Records amedai kuwa amepata inspiration ya kufanya muziki tofauti kutoka kwa nyimbo za Darassa, husasan anthem yake, Muziki.

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV Ijumaa iliyopita, Majani amesema wengi walikuwa wakimtaka atengeneze nyimbo kama za Darassa lakini hakutaka kukopi, na badala yake alitumia kama inspiration kufanya muziki wa aina tofauti.

Amesema alichopenda kwenye nyimbo za Darassa ni urahisi katika namna anavyoandika na kudai kuwa ‘simplicity siku zote inauza.’ Producer huyo ameachia wimbo wa kundi lake liitwalo Bongolos, Wape.

Comments

comments

You may also like ...