Header

Barcelona na Bayern hawana uvumilivu- Guardiola

Kocha mkuu wa Manchester City,Pep Guardiola amedai kuwa klabu zake za zamani Barcelona na Bayern Munich zingemtupia virago kama angepitia kipindi kigumu kama alichakabiliana nacho msimu huu akiwa Uingereza.

Kocha huyo mkongwe mwenye Umri wa miaka 46 ametwaa mataji 21 katika kipindi alichofanya kazi kama kocha Hispania na Ujerumani, na ameshindwa kutwaa taji Ligi Kuu Uingereza.

Akizungmza na kituo cha Talk Sport Pep amesema kuwa“Presha niliyokuwa nayo nilipowasili Barcelona, nikiwa sina cha kutetea katika klabu, kama nisingeshinda ndani ya miezi sita, ningetupiwa virago hata Bayern pia hivyo wasingekuwa wavumilivu”

Mpaka sasa Man city wamebakia na  michezo miwili ya kumaliza Lig Kuu wakikabiliana na Westbrom na kumaliza ligi na Watford

Comments

comments

You may also like ...