Header

Cassper Nyovest uso kwa uso na Jidenna

Msanii wa muziki wa rap kutoka Afrika Kusini na mkali wa ngoma ‘Tito Mboweni’ Cassper Nyovest amemtaja staa wa ngoma ya ‘Classic Man Remix’ aliyomshirikisha rapa Kendrick Lamar ‘Jidenna’ walipo kukutana UK katika #OneAfricaMusicFest hata Cassper kufurahishwa kusikia kuwa Jidenna ni msanii anayefatilia muziki wake kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita taarifa ambayo inaonekana kuwa Cassper ameipata kupitia mazungumzo yao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Cassper Nyovest alipost picha akiwa na staa huyo ‘Jidenna’ na kuambatanisha maneno ambayo yalidhihirisha kuwa muziki anaofanya kwa kipindi chote hasa cha miaka miwili iliyopita umemfikia Jidenna hata kuongeza kuwa wamefanya mazungumzo mafupi kuhusu kazi.

“Nimekutana na Jidenna jana usiku. Alisema amekuwa akifatilia muziki wangu miaka miwili iliyopita. Tumezungumza kiasi kuhusu kazi. Tazama” Alipost Cassper.

Met @jidenna last night. He said he been checking my music for 2 years now. Spoke briefly about work. Look out .

A post shared by Refiloe Phoolo 🇿🇦 (@casspernyovest) on

Hata hivyo Cassper Nyovest anategemewa kutua nchini Tanzania ambapo anakutana katika jukwaa moja na rapa kutoka Marekani Future, Diamond Platnumz kutoka Tanzania na wasanii wengine wakongwe na wakali kutoka Tanzania watakaopata nafasi ya kutumbuiza tarehe 22 ya mwezi Julai mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.

Comments

comments

You may also like ...