Header

Msuva hati hati kuwakabili Toto Africa Leo

Mshmbuliaji mwenye njaa ya Magoli Simon Msuva, anaweza kukosa mchezo wa leo Jumanne dhidi ya Toto Afrika, baada ya kupasuka na kushonwa nyuzi 4 kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mbeya City

Dakatari wa  Wanajangwani Edward Bavu, ameimbia DizzimOnline kuwa Msuva anaweza kuikosa mechi ya leo kutokana na majeruhi aliyoyapata kwenye mchezo dihidi ya Mbeya City huku Yanga wakiibuka na Ushindi wa goli 2-1

“Amepasuka na tumemshona nyuzi nne, kuhusu kucheza itategemea na maendelea ya kidonda ”amesema Bavu

Msuva alifunga dhidi ya Mbeya City na kuwa goli la 14 msimu huu na kumweka katika nafasi nzuri ya kutetea kurudia mafanikio aliyoyapata msimu wa 2014/15 alipokuwa mfungaji bora kwa kufunga mabao 17 na Amissi Tambwe kushika nafasi ya pili akiwa na mabao 14.

Comments

comments

You may also like ...