Header

Simba Sc yapigana kumrudisha Mo kundini

Mohammed Dewji jina maarufu hapa mjini “Mo” ameamua kujitoa katika suala la mchakato wa mabadiliko baada ya klabu ya Simba kuingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya ubashiri ya SportPesa.
Dewji ameonesha  kukasirishwa baada ya uongozi kutomshirikisha yeye pamoja na wajumbe wengine wa kamati ya utendaji, jambo aliloliita kutoaminiana miongoni mwao.
 Chanzo chetu kutoka mitaa ya Msimbazi kinasema kuwa“Uongozi utakutana na Mo, itakuwa leo au kesho ili kulimaliza suala hilo. Kinacholengwa ni kuonyesha busara baada ya matatizo yaliyotokea kuyamaliza na kujiandaa kwa pamoja kuelekea fainali ya kombe la Shirikisho”
MO ambaye alikuwa msaada mkubwa hapo klabuni lakini kitendo kilichofanywa na viongozi wa Simba akikumfuraisha na kuamua kukaa pembeni lakini tayari uongozi wa Simba unajipanga kumrudisha kundini.

Comments

comments

You may also like ...