Header

Tamthilia ya Quantico ya Priyanka Chopra yaongezewa Episode 13 mpya

Mafanikio ya staa wa Bollywood, Priyanka Chopra yanazidi kushika mizizi Marekani. Mrembo huyo mwenye miaka 34 na anayeigiza tamthilia ya Quantico kupitia kituo cha runinga cha ABC, ameongezwa episode 13 za msimu mpya wa 3.

Tangazo hilo limetolewa Jumatatu hii baada ya kuwepo hofu iwapo tamthilia hiyo itaendelea.

Kupitia Twitter, Priyanka ameandika, “So excited about the season 3 pick up for #Quantico congrats to everyone who made it happen! #AlexParrish will be back soon.’

Show hiyo itaendelea kutayarishwa jijini New York. Utazamwaji wa Quantico umeendelea kushuka kwa kasi ukilinganisha na ilivyoanza mwaka 2015.

Comments

comments

You may also like ...