Header

Breaking: Dogo Mfaume afariki Dunia.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ‘Dogo Mfaume’ baada ya matibabu ya muda kufuatia kudhohofika kwa matumizi ya madawa ya kulevya taarifa zinasema kuwa amefariki dunia mchana wa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Akizungumza na Dizzim Online, Mkurugenzi wa kituo alichokuwa akitibiwa cha ‘Missana Foundation’ kilichopo Kigamboni Pili Misanna amesema kuwa hali ya Dogo Mfaume ilishaanza kuwa nzuri na aliendelea na matibabu ambapo siku ya Ijumaa ya wiki hii alikuwa katika taratibu za kufanyiwa upasuaji wa kichwa kumuondolea uvimbe aliokuwanao kwenye ubongo.

Kwa niaba ya Dizzim Online tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msima huo.

#RIP #DogoMfaume.

Comments

comments

You may also like ...