Header

Japan kuzindua magari yanayopaa kwenye Olimpiki 2020

Japan imejipanga kuzindua magari yanayopaa kwenye michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwaka 2020 kwenye mji mkuu wake, Tokyo. Kampuni ya Toyota ndio inayofadhili mradi huo kuleta gari ndogo zaidi duniani inayopaa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya drone.

Watengenezaji wake wanatarajia kuizindua gari hiyo mwishoni mwa mwaka 2018 kwa lengo la kuitumia kung’arisha ufunguzi wa mashindano hayo mwaka 2020.

Gari hiyo ni wazo la Cartivator Project, kundi la engineer vijana waliopo kwenye shule ya Aichi Prefecture. Gari hilo limepewa jina, SkyDrive na litakuwa na matairi matatu na propeller nne. Gari hiyo inatarajiwa kusafiri kwa mwendo wa mile 62 kwa saa juu ya futi 32.8 na kutua kwa mwendo wa maili 93 kwa sasa.

Comments

comments

You may also like ...