Header

Jay Z na Beyonce sasa ni couple yenye ubilionea rasmi

Beyoncé na Jay Z ni couple yenye ubilionea rasmi. Kwa mujibu wa orodha ya Forbes ya America’s Wealthiest Self-Made Women iliyotoka Jumatano hii, Beyoncé, 35 amekusanya utajiri wa dola milioni 350. Kwa upande wa Jay Z, amekusanya utajiri wa dola milioni 810 na hivyo kwa pamoja kuwa na utajiri wa dola bilioni 1.16.

“I’m never satisfied,” Bey aliiambia FORBES. “I’ve never met anyone that works harder than me in my industry.”

Fedha nyingi za Bey zimeongezeka kupitia ziara yake ya mwaka jana, Formation World Tour, ambayo iliingiza takriban dola milioni 250 na mauzo ya album yake ya sita, Lemonade pamoja na miradi mingine.

Jay Z anaendelea kutengeneza fedha kupitia label yake ya Roc Nation, mtandao wa Tidal na biashara zingine.

Comments

comments

You may also like ...