Header

Man United nje ‘top four’ ya Ligi Kuu Uingereza

Ligi Kuu ya England inafikia mwisho Jumapili ya wiki hii baada ya Chelsea kunyakua ubingwa wa msimu huu mapema, huku Manchester United kimahesabu ikitupwa nje katika msimamo wa kumaliza nafasi nne za juu.

Nafasi zinazofuata, ya kwanza na ya pili zimechukuliwa tayari baada ya Tottenham kujihakikishia kumaliza nafasi hiyo bila kuwa na mpinzani.

Liverpool inapewa nafasi kumaliza ya 3, 4 na 5. Pia Manchester City inapewa nafasi kumaliza 3,4 na 5 huku Arsenal wakipewa nafasi kumaliza 3, 4, 5 na 6.

Manchester United imebakiza matumaini ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya kupitia mechi yao ya fainali ya Ligi ya Europa itakayopigwa Mei 24.

Hata hivyo Klabu ya Everton hata wakifungwa au wakishinda mchezo wao wa mwisho watabaki kuwa nafasi ya 7 tu.

Comments

comments

You may also like ...