Header

Rayvanny azungumzia kuvuja kwa ngoma yake na Khaligraph Jones

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya WCB anayesumbua anga na ngoma yake ya ‘Zezeta’ Rayvanny amezungumzia kile kinachoonekana kama ni uvujaji wa ngoma aliyoshirikishwa na rapa kutoka Kenya Khaligraph Jones a.k.a OG Papa Jones.

Akipiga stori na Dizzim Online kuhusu wimbo huo wa Khaligraph unaokwenda kwa jina la ‘Chali ya ghetto’ Rayvanny amesema kuwa anachojua kuhusu wimbo huo ni kuwa haujavuja bali kilichotokea Khaligraph aliutambulisha wimbo huo katika moja ya kituo cha runinga ambako wengi wao kwa mara ya kwanza waliweza kuisikia kupitia pale ingawa Rayvanny hakujua kama inaruhusiwa kufanya hivyo kabla ya ngoma hiyo kutoka rasmi.

“tulifanya kolabo na Khaligraph na tukashoot video pia Kenya lakini kilichotokea ni kwamba alikuwa kwenye kipindi kimoja cha Tv akawa ameiperfom ngoma so watu wengi wakaijua kupitia pale sio kwamba imevuja…mimi mwenyewe nilikuwa sina taarifa kama inaruhusiwa aiperform before hatujaitoa so ni menejimenti pia tutakaa chini tujue inakuwa vipi kwasababu tulikubaliana kufanya kolabo na pia kwenye utoaji lazima tuwe na makubaliano pia”.

Aliendelea “Lakini kwasababu ngoma ni ya kwake na yeye kanishirikisha mimi nafikiri kwa upande wake anaweza kuwa na maamuzi yeye lakini pia kwenye menejimenti yangu kuna maamuzi pia lazima ambayo yanatakiwa yawepo kutokna na ambavyo tulikuwa tumekubaliana pia” Amesema Rayvanny.

Akizungumzia makubaliano ya wimbo huo Rayvanny amesema kuwa ngoma itatoka kulingana na mikakati iliyopangwa na kuongeza kuwa mashabiki wangoje kazi ambayo imekamilika kabisa kulingana na makubaliano katika ya Khaligraph na menejimenti ya Rayvanny ya WCB.

Hata hivyo rapa Khaligraph kwasasa anafanya poa na kazi yake mpya inayokwenda kwa jina ‘Toa Tint’ huku Rayvanny ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki kuchaguliwa katika tuzo kubwa duniani za BET za mwaka huu katika kipengele cha Best International View’s Choices.

Comments

comments

You may also like ...