Header

Snoop Dogg awataja wasanii wake 3 anaowakubali siku zote

Rapa kutoka Marekani Snoop Dogg mkongwe anayetajwa kuendelea kufanya vizuri katika muziki wa rap kwa miongo miwili sasa anayetarajiwa kuachia album yake ya 15 inayokwenda kwa jina ‘Neva Left’ amewataja marapa wake anaowakubali kwa muda wote.

Akipiga stori katika kipindi cha Jimmy Kimmel Live’ kinachoongozwa na Jimmy Kimmel rapa Snoop aliulizwa kuwa ataje marapa anaowakubali kwa muda wote ambapo alimbainisha rapa Slick Rick, Ice Cube na kumalizia kuwa wa tatu ni yeye mwenyewe.

Rapa huyo kabla ya kutoa orodha hiyo ya wasanii wa muziki wa rap anaowakubali Snoop alidai kuwa msukumo wa kufanya muziki aliupata kupitia wimbo wa ‘Super Rhymes’ wa Jimmy Spicer na kusema kuwa aliandika wimbo wake wa kwanza uliokwenda kwa jina ‘I’m a Poet’ wimbo ambap anadai aluandika akiwa na umri wa miaka 11 au 12 lakini alipoulizwa kama anakumbuka mistari ya wimbo huo Snoop alijibu kuwa ulikuwa ni wimbo wnye uandishi mibovu sana.

Hata hivyo ujio wa album yake mpya ya ‘Neva Left’ unategemewa aichiwe rasmi tarehe 19 mwezi Mei mwaka huu.

Hii ni orodha ya nyimbo za album ya Snoop Dogg.

 1. Neva Left
  2. Moment I Feared (ft. Rick Rock)
  3. Bacc In da Dayz (ft. Big Tray Deee)
  4. Promise You This
  5. Trash Bags (feat. K CAMP)
  6. Swivel (feat. Stresmatic)
  7. Go On (feat. October London)
  8. Big Mouth
  9. Toss It (ft. Too $hort & Nef The Pharaoh)
  10. 420 (Blaze Up) [ft. Devin the Dude, Wiz Khalifa & DJ Battlecat)
  11. Lavender (Nightfall Remix) [ft. BADBADNOTGOOD & KAYTRANADA] 12. Let Us Begin (ft. KRS-One)
  13. Mount Kushmore (ft. Redman, Method Man & B-Real)
  14. Vapors (DJ Battlecat Remix) [ft. Charlie Wilson & Teena Marie] 15. Still Here
  16. Love Around the World (ft. Big Bub)

Comments

comments

You may also like ...