Header

Joh Makini awapongeza Directors wa bongo na kuwapa njia ya kumshawishi afanye nao video

Rapa ‘John Simon’ a.k.a Joh Makini anayefanya poa na dundo la ‘Waya’ amezungumzia viwango vya waongozaji na changamoto zilizopo katika utengenezaji wa video za muziki Tanzania na kutoa sababu za kwanini anaendelea na mfumo wa kufanya video zake na kufuata waongozaji nje.

Akizingumzia kile kinachoonekana kuwa amewatenga waongozaji wa video za muziki wa Bongo kwa kiasi kikubwa kutokana na kufanya video nyingi nje ikiwa ni pamoja na video ya wimbo wake wa ‘Waya’ video amayo ameshootia nchini Afrika Kusini chini ya uongozaji wa Director Nic na video inayosubiriwa sana ya wimbo wake alimshirikisha Davido kutoka Nigeria na kulitetea hilo kuwa kutokana na malengo na nafasi aliyofikia nakila sababu ya kuendelea kwenda nje kutafuta ananchojisikia kupata ili uendelea kulinda thamani ya kiwango cha muziki wake.

Mimi siwezi kukuficha kwamba natafuta ubora, na standard ambayo nime-set katika muziki wa Joh Makini. Inanilazimisha kuendelea kwenda juu sio kurudi chini…waongozaji wa Bongo nawaamini sana lakini nakuwa comfortable nikiwa nafanya video na ma-director wa nje mara nyingine kwasababu nakuwa sina stress, nakuwa napata kila kitu on set na wao wanakuwa wanafanya kila kitu alafu very professional” Alisema Joh Makini.

Akitia neno kama ushauri juu ya hali halisi kutokana na hatua zake za kuupelekea muziki wake hata kupeperusha bendera ya muziki wa Tanzania kimataifa kwa ujumla Joh amesema kuwa kwa mwendo wa waongozaji kama wataongeza kasi yao muda si mrefu wasanii ambao wanaelekea viwango vya kimataifa wataachana na mfumo huu wa kwenda nje ya nchi kwa lengo la kufuata waongozaji bali kama itawalazimu iwe hivyo wataenda nje ya nchi kufuata mazingira na vitu vya tofauti na sio waongozaji tofauti na asilimia kubwa ya hali ilivyo kwa sasa.

“lakini so far wanafanya kazi nzuri naona video za Hascana, naona za Armando(Khalifan), naona video za wale Kwetu Videos wanatia moyo sana naamini soon tutaacha kusafiri kwa ajili ya Ma-director, tutakuwa labda tunasafiri tu pengine kufuata mazingira na vitu vingine kama hivyo” Aliongeza Joh makini alipokuwa akingea na 255 ya Clouds Fm.

Comments

comments

You may also like ...