Header

Ommy Dimpoz anasafiri kama bilionea

Ukiweka pembeni muziki, kama ni kutaja kitu ambacho Ommy Dimpoz anakifanya kwa weledi wa hali ya juu, basi ni kuishi maisha ya kifahari, ulaji bata na mitupio ya pamba kali, walau kwa jinsi anavyoonekana kwenye Instagram.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, hitmaker huyo wa Kajiandae, alikuwa Marekani kushuhudia mchezo wa kikapu wa fainali za Eastern Conference kati ya Cleveland Cavaliers na Boston Celtics (117 -104).

Na sasa katika kile ambacho kinaonekana kuwa amekula flight kurudi Bongo ama kokote anakoelekea, Ommy ameonesha kuwa hapandi ndege kama mtu wa kawaida, ana fly kama bilionea.

Amepost kwenye Instagram picha akiwa kwenye business class ya ndege aliyokuwamo, headphone kichwani akiuchapa usingizi angani, kwa raha zake. “😴😴😴 How was ur sleep?,” ameuliza kwenye picha hiyo ambayo amelazimika kumute comments kuepusha haters kumharibia usingizi wake.

Comments

comments

You may also like ...