Header

P-Funk asema mkewe amembadilisha kwa kiasi kikubwa ‘nimekuwa mtu wa dini sana’

Pamoja na heshima kubwa aliyoweka kwenye muziki wa Bongo Flava, P-Funk ni mtayarishaji wa muziki ambaye kwa muda mwingi amekuwa akielezewa kama the ‘bad boy.’ Hiyo ni kutokana na kuwa na historia ya kutopenda mambo ya kipuuzi, na kwa wale waliowahi kumchezea, wanajua alichowafanyia. Lakini, Majani wa mwaka 2017, si yule mwaka miaka 10 iliyopita. P amebadilika sana, na hata washkaji wake wa karibu wanakiri hilo. Nini kilichomfanya abadilike?

“I think it’s my wife as well man, she played a good part and also changing me, I have become more religious, nimemweka Mungu mbele, vitu vyote najaribu kufanya hivyo sasa hivi,” Majani amekiambia kipindi cha Chill na Sky kitakachoruka kesho saa 8 mchana kupitia Dizzim Online.

“And age, you know you grow up you start to realize ukiwa negative all the time, you actually taking away your energy, your happiness of life, you can’t be kila kitu una hasira, you trying to enjoy life, circumstances ambazo umepewa ndio hizo hizo. Kama ulidhulumiwa, you throw out of the bag unasonga mbele,” ameongeza.

Hata hivyo, Majani anasema bado hupata hasira kwa mambo mbalimbali.

“But I still get angry, you know I’m just humble. Mimi nina discipline ambayo kidogo ni ya ajabu, cha kwanza ni usafi, sipendagi kuona watoto wangu saa zingine wanafanya vitu ambavyo sivyo ambapo unakuja bibi ama mama mzazi saa zingine anaviachia and something bad happens au, those kind of things really piss me off,” ameeleza Majani.

Kingine ambacho mtayarishaji huyo wa muziki humkera, ni watu ambao hushindwa kuelewa kuwa naye ana maisha yake nje ya muziki.

“Hataki kuelewa kwamba wewe ni binadamu, wewe sio mwenyezi Mungu ambaye unaweza kusaidia kila mtu duniani na wewe mwenyewe unajaribu kujisaidia, wewe kama wewe ili uweze kuiangalia familia yako na mipango yako kwanza iende, bila mipango yangu kwenda mbele, nitawezaje kusaidia wengine? Sasa mtu ni mbishi, anaiweka kama ni lazima, ni jukumu langu kumsikiliza, kumsaidia. Unampa mtu maelekezo, unamsikiliza, unampa muda wake, lakini bado hakuelewi.”

Comments

comments

You may also like ...