Header

Tiddy Hotter na Lollipop wamkaribisha ‘Rin Marii’ kwenye Bongo Fleva

Ni kawaida katika kitengo chochote kilicho na umaarufu na chenye mafanikio kuibuka watu tofauti huku changamoto zisikose jambo ambalo liko kinyume kwa binti ambaye ameanza kunukia katika kizazi kipya cha muziki wa Bongo Fleva.

Muite ‘Rin Marii’ ambaye amengukia katika mikono ya watayarishaji wenye uwezo kubwa Tanzania katika wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina ‘Salaam’ ikiwa wimbo huo umeandaliwa na Lollipop na kuwa Mastered na muandaaji aliyeshiriki katika kufanikisha hit song ya ‘Moyo Mashine’ Tiddy Hotter huku video ya wimbo huo ikiongozwa kwa ubunifu na Director Destro kutoka Wanene Film.

Hakika kwa mwendo huu wa hii kazi yake mpya Rin ana kila dalili za kufanya vizuri kwakuwa uwezo unaonekana katika hii ya kwanza na jibu la kuwa ataendelea kufanya vizuri litakuja pindi atakapoachia kazi nyingine baada ya hii ya ‘Salaam’.

https://mkito.com/song/16679

Comments

comments

You may also like ...