Header

Fahamu umuhimu wa siku ya leo kwa Floyd Mayweather na Busta Rhymes

Kila siku ina ukubwa wake kulingana na mambo makubwa yanayotokea katika maisha ya kila siku na siku ya leo ni tarehe ambayo imebeba kitu ambacho inaaminika ni wachache wanaweza kuwa wanakifahamu.

Tarehe 20 mwezi Mei ni siku yenye kitu ambacho kinaweza kisiwe historia kwenye masikio na watu hufahamu ingawa Dizzim inaweza kukufahamisha usichokijua kuhusu siku hii ya leo hasa kwa kukurudisha miaka 17 iliyopita.

Bila shaka umevuta hisia za kurudisha miaka nyuma mpaka mwaka 2000 na kikubwa ambacho ni cha pekee ni kuwa katika kusherehekea siku ya mfanano wa kuzaliwa kwa rapa mmarekani Trevor George Smith Jr. a.k.a Busta Rhymes mwaka huo wa 2000 Bondia maarufu wa Dunia ‘Floyd Mayweather’ alipata mtoto wakike ‘Iyanna Mayweather’.

Iyanna Mayweather

 

Iyanna Mayweather akiwa na Nicki Minaj

Mtoto huyo Iyanna alizaliwa Nevada nchini Marekani na amekuwa ni mwenye bahati ya kukutana na mambo makubwa na ya kifahari kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha alionao baba yake Floyd Mayweather kwakuwa mwaka 2013 siku kama ya leo Bondia Floyd Mayweather aliandaa sherehe ya kusherekea Birthday ya wamane huyu ambapo alikuwa anatimiza umri wa miaka 14 na kikubwa alicho fanya kwa ajili yake na wote walioalikwa ni kumualika muimbaji maarufu Justin Bieber kutoa burudani fupi kwenye sherehe hiyo.

Kwa upande wa Busta Rhymes leo anatimiza miaka 45 na mbali na kushare terehe hii ya kuzaliwa na motto wa kike wa Mayweather ‘Iyanna’ pia anashare siku hii na Diamond rapa wakike anayefanya vyema Marekani ambaye ametimiza miaka 27.

Comments

comments

You may also like ...