Header

Linah na Kijacho wake waangukia dili

Msanii wa muziki wa bongo fleva kutoka Tanzania anayeendelea kufanya vyema na ngoma yake ya ‘Upweke’ ‘Linah Sanga’ zikiwa ni wiki chache ajifungue mtoto wake wa kwanza amepata ubalozi wa duka la nguo za watoto la Kids City Shopping (KCS) duka ambalo pia linauza bidhaa mbalimbali za akinamama wajawazito.

Linah ambaye wiki hii alitambulisha herufi ya mwanzo ya jina la mtoto anayemtarajia baada ya kuweka picha ya ujauzito kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika ‘Baby T on the way’,anakuwa miongoni mwa mastaa ambao watoto wao wamepata bahati ya kuwa mabalozi.

“Kwa mara ya kwanza nitazungumza na mashabiki wangu mwishoni mwa wiki hii kwa niaba ya KCS ambao ni  wauzaji wa bidhaa mbalimbali za watoto na akinamama wajawazito,” amesema Linah.

Officially pregnant ambassador CC @kids_cityshopping karibuni wote mjipatie nguo nzuri kwa watoto.

A post shared by Linah Sanga (@officiallinah) on

Aidha Linah, karibuni alimtangaza mpenzi wake anayetarajia kuwa baba wa mtoto wake aitwaye Shabani mmiliki wa Kampuni Drops Up Entertainment ambaye pia ni bosi wake, Linah amedai kuwa anafuraha kuwa mjamzito kwa kuwa ni kitu ambacho alikuwa akitamani kwa muda mrefu.

“Ninafuraha kubwa kwa sababu ni kitu ambacho kama mwanamke nilikuwa nakitamani siku zote kwamba na mimi nije niitwe mama, nafuraha nimepata mtu sahihi wa kuwa mzazi mwenzangu ambaye nitalea naye watoto,” Aliongeza Linah.

 

 

 

 

 

 

Chanzo: Mwananchi

Comments

comments

You may also like ...