Header

Sipendi mwanangu aje kuwa staa wala kujichora tattoo – Nuh Mziwanda

Msanii wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda aka baba Anyagile aliyetamba na ngoma yake ya Jike Shupa, anatamani mwanae akija kuwa mkubwa awe mtu wa kawaida tu na wala asizuzuke na ustaa wa baba yake.

Ameiambia Dizzim Online, “Mwanangu najitahidi kumtengenezea mazingira tangu mwanzo yale ambayo yeye baadaye yasije yakamkarahisha au akajiona yupo tofauti na watoto wenzie, hicho kitu cha kwanza that is why sipendi kumpublish sana kwenye mitandao ya kijamii. Pia nataka awe msomi , sitegemei mwanangu aje kufanya muziki wa Bongo Flava au mwanangu sitaki arithi chochote kutoka kwangu hata lifestyle yangu sitaki arithi.”

Pia aliongeza, “Hata kuchora tattoo sitopenda mwanangu aje achore kwa sababu naamini sio kitu kizuri ingawa mimi mwenyewe nimechora na zina maana kwangu lakini sitopenda mwanangu aje afanye hvyo,” muimbaji huyo ameiambia Dizzim Online.

Vilevile hakusita kuzungumzia muziki wake na kuwaomba mashabiki zake waendelee kumsapoti ili azidi kufika mbali zaidi.

BY DINNY NASSORO

Comments

comments

You may also like ...