Header

Stamina athibitisha mipango ya kazi na Khaligraph Jones

Rapa kutoka Tanzania Stamina, anayefanya poa na ngoma ‘Love Me’ iliyotayarishwa na ‘Bear’ chini ya ‘Kiri Records’ ndani iliyomshirikisha Maua Sama amethibitisha mipango ya kufanya ngoma na rapa kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones.

Akizungumzia uwezo wa Khaligraph hasa kupitia ngoma yake mpya ya ‘Toa Tint’ na kumkubali pia, Stamina amesema kuwa karibuni Khali atatua nchini Tanzania na moja ya mambo ambayo yatahusika atakapokuwa nchini ni mipango ya wawili hao kufanya ngoma ya pamoja.

“kwanza Khaligraph mimi hapa ni mmoja ya marapa wanotokea 254 ambao mimi nawapenda na sio tu nawapenda, good thing ni kwamba anakaribia kuja Tanzania na moja kati ya plans ni kufanya naye ngoma pia” Alisema Stamina.

Hata hivyo Stamina ametangaza rasmi kuwa Producer Maneck ni meneja wa muziki wake hata kusema kuwa ameongeza watu ambao wanahusika na mambo yote muhimu ya kumtengeneza na kumuweka katika mazingira kama msanii aliyepiga hatua chini ya kampuni inayojulikana kama Babaz Entertainment.

Comments

comments

You may also like ...