Header

Snoop Dogg atangaza kufanya Injili

Rapa mmarekani na mkongwe Snoop Dogg amebainisha mipango yake ya kufanya kazi zenye maudhui ya ijili katika muziki wake.

Akizingumza na Beat 1 Radio, Snoop amesema kuwa ni muda tangu kusikika kwake katika muziki wa kufoka foka unaozungumzia maisha ya kawaida hasa ya kibiashara na sasa ni wakati wa kufanya injili kwasababu wazo hilo amekuwa nalo kwa muda mrefu.

“…Wao hili limekuwa kichwani kwangu…” alisema “sikuwa nimeamua kulifanyia kazi kwasababu ya kuwa kwenye mambo mengine ya kibiashara zaidi na kimiziki huku nikifanya mambo ya hapa na pale. Lakini ni jambo ambalo nimekuwa nikiliwaza kwa muda mrefu. Nahitaji kulifanyia kazi sasa” Aliongeza Snoop Dogg.

Hata hivyo Snoop tayari ana idadi ya baadhi ya watu ambao anafikiria kuwashirikisha katika ngoma za injili atakazo fanya ambao ni pamoja na Faith Evans, Charlie Wilson na Jeffery Osborne na wengine ambao atawahitaji kwa baadae.

Katika hili Snoop ataonekana tena akifanya kitu cha pekee ambapo mwaka 2013 alibadilisha jina na kuanza kujiita Snoop Lion kama maandalizi ya kuachia album yake ya ‘Reincarnated’. Snoop kwasasa sokoni ameachia album yake mpya inayofahamika kama ‘Neva Left’ iliyoingia sokoni terehe 19 Mei mwaka huu.

Comments

comments

You may also like ...