Header

Albert Msando aomba radhi kwa video iliyosambaa akichezeana na Gigy Money

Mwanasheria maarufu nchini, Albert Msando, amejikuta kwenye kiti moto baada ya kusambaa kwa video anayoonekana akila bata na mrembo wa video za muziki, Gigy Money. Kwenye video hiyo wakiwa kwenye gari na Gigi, Msando anaonekana akimshikashika Gigi sehemu za siri. Na sasa Msando ambaye ana mke, ametumia Instagram kukiri kosa lake na kuomba radhi.

“Nikikaa kimya nitakua mnafiki. Nimekosea,” ameandika. “Kilichotokea hakikupaswa kutokea. I will be a man enough and say sorry kwa wote ambao nimewakwaza na kuwaangusha. Am so sorry. But the beauty of all this is we all are human. Kuna watu ambao wamekuwa wepesi kuhukumu. Siwalaumu. Ni sawa na ni haki yao. I made a stupid mistake. I take full responsibility. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee. It could have been worse. And to all those who took time to text I appreciate. Thats friendship. #TheDon #Hennessy #TheClip.”

Naye rapper Nick wa Pili amemtetea Msando kwa kuandika: Unapopatwa na jambo kubwa ni vyema kujitokeza na kulisemea…@albertomsando….. wote tuna upande wetu wa giza.. ndio mana tunaomba na kutubu kila siku.. ndio maana ya kanisa kuwa wazi kila siku na kuwapo na sala tano……. Amekosea @albertomsando.”

Comments

comments

You may also like ...