Header

BASATA lalaani picha za Ben Pol, ‘tutazungumza naye kujua kama ana tatizo la akili’

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania, BASATA, Godfrey Mngereza amelaani picha ya utupu ya msanii wa R&B, Ben Pol ambayo imezua tafrani kubwa kwenye mitandao ya kijamii. Akizungumza na Dizzim Online, Mngereza amesema sanaa ya Tanzania bado haijafikia zama za kufanyika kitendo kama hicho na kwamba BASATA linakilaani.

“Kwa tamaduni zetu bado hatujafikia hapo ni wengine huko ambao wanaruhusu,” amesema. “Hiyo ni moja, pili ni kitendo ambacho baraza inakilaani lakini kwa utaratibu wa baraza kama baraza tutamtafuta Ben Pol tuweze kumsikia mwenyewe kwamba zile picha kweli amepost yeye au kuna kitu kingine kwa sababu teknolojia imekwenda mbali sana siku hizi kwahiyo tutamsikiliza anahusika vipi moja kwa moja. Lakini kimsingi kwa ujumla wake baraza inakilaani na tutaendelea kumtafuta Ben Pol kuzungumza naye kwa sababu ni haki yake kusikilizwa katika hilo.”

Ameongeza Mngereza,” Pia naungana na wasanii waliolaani kitendo hiko ambacho ni cha ajabu sana na baraza kwa mamlaka yake kama mzazi haiwezi kukaa kimya lazima tujue kama ana tatizo la akili au maadili limemkumba Ben Pol.”

Pia Mngereza amewaomba wasanii wa Tanzania kwa upande wa muziki wafanye muziki mzuri wasitegemee kiki.

Comments

comments

You may also like ...