Header

Beyonce afanya baby shower yenye theme ya Kiafrika, alipaka henna tumbo lake

Jumamosi, Beyonce alialika ndugu, jamaa na marafiki kwenye baby shower yake aliyoipa jina, Carter Push Party na kuipa muonekano wa tamaduni za Kiafrika.

Aliwaalika marafiki zake Michelle Williams na Kelly Rowland pamoja na mastaa wengine wakiwemo, Serena Williams, Tina Knowles, La La Anthony, Vanessa Bayer. Hafla hiyo ilifanyika huko Beverly Hills na palionekana ballon zilizoandikwa ‘Carter Push Party’ na ‘Twinning.’

Beyonce alijichora henna tumboni mwake na kuvalia nguo na kilemba cha vitenge na huku mumewe Jay Z akivalia kibaragashia kichwani. Muimbaji huyo anatarajia kujifungua watoto mapacha.

Tazama picha zaidi hapo chini.

Comments

comments

You may also like ...