Header

Lava Lava amaliza mwaka mzima WCB bila kuonana na Diamond Platnumz

Msanii mpya wa kizazi kipya kutoka lebo ya muziki Tanznaia WCB ‘Abdul Juma Mangala’ a.k.a Lava Lava mwenye ujio mpya wa ngoma inayokwenda kwa jina ‘Bora Tuachane’ amesimulia kipindi chote alichotembelea mazingira ya Ofisi na studio za WCB bila kuonana uso kwa uso na Diamond Platnumz.

Akizungumzia safari ya muziki kiasi cha kukata tamaa mpaka kukutana na uongozi wa studio hizo na Diamond Platnumz, Lava Lava amesema kuwa haikuwa rahisi kufikia hatua ya kufanya kazi na WCB hata kusimulia siku jinsi alivyoruka mtego wa kumuuzia wimbo Diamond Platnumz.

“lakini cha kushangaza mimi nimekaa miaka miwili WCB, mwaka mmoja mzima Diamond sijakutana naye niko hapo hapo…mwaka mzima…unajua mtu akienda WCB ndoto yake ya kwanza ni kumuona Diamond…hata siku moja sijamuona” Amesema Lava Lava aliyekaa WCB kwa kipindi cha miaka miwili akingoja na kufuata taratibu za kufikia kutoka kama msanii anayefanya kazi rasmi chini ya usimamizi.

Hata hivyo Lava Lava kwasasa ni miongoni mwa wasanii Tanzania ambaye ameungana na timu kubwa ya wasanii wa WCB ambao ni pamoja na Diamond Platnumz, mwenye, Rich Mavoko, Harmonize, Rayvanny na Queen Darleen.

Comments

comments

You may also like ...