Header

Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ achaguliwa kama mchezaji Bora

Beki wa kulia wa klabu ya Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Mei kwa msimu wa 2016/2017.

Kufikia kuimbuka na ushindi huo ‘Tshabalala’ katika  mwezi Mei kulikuwa na raundi tatu ambazo Hussein alicheza kwa dakika zote 270 na kutoa mchango mkubwa katika kuisadia timu yake kubaki katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Mbali kutajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi pia ni mchezi aliyeonesha  nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopewa onyo la aina yoyote.Kwa kushinda tuzo hiyo huku wachezaji wengine walioshinda tuzo za mwezi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 ni John Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Msuva wa Yanga (Oktoba) na Riphat Said wa Ndanda (Novemba).

Hata hivyo wachezaji wengine ni Method Mwanjali wa Simba (Desemba), Juma Kaseja wa Kagera Sugar (Januari), Hassan Kabunda wa Mwadui (Februari), Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar (Machi) na Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting (Aprili).

Kwa ushindi huo Hussein amewashinda wachezaji kama Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam FC.

 

 

 

 

BBC

Comments

comments

You may also like ...