Header

Q-Chilla aelezea mazungumzo yalipofikia kati yake na WCB

Jumatatu hii, WCB wamemtambulisha msanii wao mpya aitwaye Lava Lava na kuachia ngoma yake mpya, Bora Tuachane. Hata hivyo, mmoja kati ya watu tuliokuwa tunategemea kuwa siku moja asajiliwe na label hiyo ni Q-Chilla. Imefikia wapi?

Kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM, Q amesema, “WCB is an organization, is an institute of many people with many creativities and have done a lot of things and I respect that. Ila wao wako chini kukaa kufikiria nini wafanye na mimi nina mambo yangu siwezi kuacha kwasababu wao wanafikiria.”

Q Chilla aliongeza kwa kusema , “All in all I know is kwamba this music is growing and at the point we are going to meet at the central point. Ni uhai tu watu wasubirie project yangu mpya soon to be released. Ni mapema kuizungumzia na mwezi wa Ramadhani unakuja tufunge tumalize halafu tuangalie nini kinakuja.”

BY SASHA NKYA

Comments

comments

You may also like ...