Header

19 wauawa kufuatia shambulio la kigaidi kwenye show ya Ariana Grande, Manchester

Takriban watu 19 wamepoteza maisha na wengine 59 kujeruhiwa kufuatia shambulio la bomu la kujitoa mhanga lililowalenga vijana waliokuwa wakitoka kwenye tamasha la muziki kwenye uwanja wa Manchester usiku wa jana nchini Uingereza.

Shambulio hilo limefanyika kwenye show ya mwanamuziki wa Marekani, Ariana Grande.

Baada ya mlipuko huo kusikika, vijana waliokuwa wakitoka kwenye uwanja huo unaochukua watu 21,000, walianza kukimbia hovyo ambapo mashuhuda wanasema ilikuwa kama eneo la vita. Tukio hilo limetokea saa 4 na dakika 35 usiku.

Muda mfupi baada ya mlipuko huo, Ariana Grande alitweet: From the bottom of my heart, I am so so sorry. I don’t have words.’ Meneja wake, Scooter Braun aliongeza, ‘We mourn for the children.’

Shuhuda mmoja amedai kuwa Ariana alikuwa amemaliza wimbo wake wa mwisho ndipo mlipuko uliposikika. “Ghafla kila mmoja akaanza kupiga kelele na kukimbilia mlango wa kutokea. Tulisikia sauti za king’ora cha polisi na gari ambulance. Ilikuwa inatisha,” alisema.

Aliongeza, “Kulikuwa na maelfu ya watu wakijaribu kutoka nje kwa wakati mmoja. Wote walikuwa wakipiga kelele na kulia. Eneo zima lilikuwa na moshi na linaloungua. Mlipuko ulisikika kama ulikuwa ndani ya jengo sehemu.”

Comments

comments

You may also like ...