Header

Madee: Kusimamia msanii si kazi ya lele mama

Rais wa Manzese ambaye mpaka leo hajaapishwa, Madee amezungumzia kuhusu kumsimamia msanii mwingine ukiachana na Dogo Janja pamoja na changamoto za kusimamia wasanii.

Ameiambia Dizzim Online, “Watoto wapo wengi sana ambao wanatamani kufanya kama anavyofanya Dogo Janja, ila tunaangalia time na wapo wengi wenye vipaji vikubwa sana, so time ikifika nitamleta kwenu na watu waweze kumjua. Kwa sasa tunatakiwa kuwa makini sana juu ya hilo.

Kuhusu ugumu wa kusimamia mtoto wa mtu kwenye muziki, Madee amesema,”Ugumu unakuja pale unapoamua kumlea mtoto ambaye sio wangu kwa sababu anakuja na tabia zake ambazo amekua nazo, kwahiyo unapoamuamua kumchukua wewe lazima umweke kwenye mstari kwa tabia ambazo unazitaka wewe. Kwahiyo cha kwanza natakiwa kumbadilisha kwenye nidhamu kitu ambacho kinakuwa kigumu sana.”

Aliongeza na kusema, “Katika kusimamia huko sipendi kuanza kumsimamia mtu mzima, nataka nibaki kule kule na watoto kwasababu nahisi tutashindwana tu maana wanasema samaki mkunje angali mbichi, sasa kwa mkubwa nitamkunja vipi? Kwahiyo nataka nibaki na watoto wakulie mikononi mwangu.”

Madee kwa sasa bado anafanya vizuri na wimbo wake Hela.

Comments

comments

You may also like ...