Header

Nay wa Mitego aomba ufafanuzi juu ya nini wasanii wanatakiwa kuimba

Msanii wa muziki wa Rap kutoka Tanzania na hitmaker wa ngoma ya ‘Wapo’ Nay wa Mitego ameweka wazi kuwa hajawahi kujihusisha na muziki wa siasa kama baadhi wanavyo tafsiri muziki wake bali anafanya muziki unaozungumzia matatizo yanayoizunguka jamii yake na maisha ya kila siku ya watanzania.

Nay kama msanii anayeguswa kwa namna moja ama nyingine amautetea muziki wake kufuatia kauli ya Waziri mwenyedhamana ya sanan Dkt Harrison  Mwakyembe bungeni  kuhusu wasanii kutenganisha muziki wao na masuala ya siasa huku akibainisha kuwa hajawahi kufanya muziki wenye maudhui ya siasa.

“…siasa ni maisha ya watu ambayo wanaishi kila siku, muziki pia ni maisha ya watu ambayo watu wanaishi kila siku so anahitaji kutoa ufafanuzi wa kutosha juu ya hili. Siasa ni maisha ya watu, muziki ni maisha ya watu, mimi binafsi ninachoamini sijawahi kuimba wimbo wa siasa hata siku moja. Mimi huwa naimba maisha ya watu ambayo yanaendelea kila siku na ndio maana wengi thubutu kusimama upande wangu endapo linapotokea tatizo lolote” Alisema Nay kupitia E News ya Ea Tv.

Vile vile Nay wa Mitego amemuomba Dkt Mwakyembe kutoa maelezo zaidi ya kina kuhusu kauli yake ya kuwa wasanii wasihusishe muziki wao na siasa kauli iliyozua mjadala hata wengi wakihisi kuwa inawezekana ni kauli ambayo inatoa tahadhari kwa wasanii watakao onekana kujihusisha.

“Labda Mheshimiwa waziri anatakiwa kufafanua zaidi juu ya hili ili watu watambue kipi hawatakiwi kuimba, kipi wanatakiwa kuimba kwasababu siasa ni maisha ya watu ya kila siku na muziki wa hip hop ni maisha ya watu ya kila siku” Aliongeza Nay.

Hata hivyo Nay nje ya hayo yote ameongeza kuwa hayuko tayari kubadilisha haina ya muziki anaofanya bali ataongeza ubunifu zaidi kwakuwa anajua ni nini mashabiki wake wanahitaji kutoka kwake.

Comments

comments

You may also like ...