Header

Nimejiuzulu ACT sababu nimeshindwa kuwa mfano kwa viongozi wengine na wananchi – Msando

Mwanasheria maarufu nchini, Albert Msando, amejiuzulu nafasi yake kama mshauri wa chama cha ACT. Hatua hiyo imetangazwa na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe. Msando amechukua uamuzi huo baada ya kusambaa mtandaoni kwa video inayomuonesha akichezeana na mrembo wa video, Gigy Money.

Video inayomuonesha Msando ambaye ameoa akiwa na mwanamke mwingine imesambaa pia. Tayari alishaomba radhi kupitia Instagram. Kwenye video aliyojirekodi, Msando amesema amejiuzulu kwa sababu ameshindwa kuwa mfano kwa viongozi wengine na wananchi kwa ujumla.

“Siwezi kuwa naongea au kusimamia kitu ambacho siwezi kukiishi. Kwahiyo uamuzi wangu wa kujiuzulu uko purely based kwenye fact kwamba naamini kama kiongozi unawajibika kuchukua hatua unapokosea.”

Kupitia Facebook, Zitto ameandika:

Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo. Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu kutoka katika barua yake, “kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka.” Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama. Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.
Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama – ACT Wazalendo
Dar es salaam
Mei 23, 2017

Comments

comments

You may also like ...