Header

Video ya Melanie akikataa kushikwa mkono na mumewe Donald Trump yawa gumzo

Kuwa Rais wa taifa kubwa duniani, Marekani na pia kuwa bilionea hakumsaidii Donald Trump kuyanunua mahaba ya mkewe, Melanie.

Katika kile kinachoonekana kuwa wawili hao wanaishi ndoa ya maigizo, Melanie alishindwa kujizuia kuupotezea mkono wa mumewe aliyetaka kumshika kuonesha wanapendana wakati wakiwasili jana mjini Tel Aviv, Israel kwa ziara ya kikazi.

Video hiyo inaonesha wakiwa wanashuka toka kwenye ndege ya Air Force One na Donald akataka kuushika mkono wa first lady wakati wakitembea. Lakini Melanie anaonekana kuutosa mkono wa mumewe akigoma kushikwa.

Tukio hilo liligeuka gumzo kwenye Twitter huku watumiaji wa mtandao huo wakimkejeli Trump kutokana na jinsi uhusiano wake na mkewe ulivyo. Mke wa John Legend, Chrissy Teigen alitweet video hiyo na kuandika, “I kinda dig how much she hates him.”

Comments

comments

You may also like ...