Header

Young D akataa kuwepo kwa ushindani katika muziki Tanzania

Rapa kutoka Tanzania anayefanya vyema na ngoma ‘Bongo Bahati Mbaya’ Young D amekataa kuwepo kwa hali ya ushindani katika muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania kwasasa.

Akizungumzia hali ya ushindani hasa katika kipindi ambacho ameachia wimbo wake wa BBM chini ya simamizi wa Mr. T Touch, Young D amesema kuwa kwasasa kuna watu wengi katika muziki lakini hakuna ushindani kabisa.

“hamna ushindani kabisa sasa hivi kwenye muziki wa bongo fleva…hamna, sasa hivi hamna ushindani, sasa hivi zinatoka nyimbo ishirini unapita wimbo mmoja unasema kuna ushindani.” Alisema. Inatakiwa ukisema kwenye ushindani inatakiwa nyimbo kama tano zinakimbizana ambazo unaweza kusema kuna ushindani sasa watu wamerelax sana. Sasa hivi muziki una watu wengi ila hakuna ushindani” Aliongeza Young D alipokuwa akihojiwa a Tbc Fm.

Hata hivyo mbali na Young D kusema hivyo, Producer Mr. T Touch amesisitizia katika hilo na kusema kuwa kuwa ni sawa na studio zinazo fanya muziki Tanzania ni nyingi lakini ni chache zinafanya vizuri kwakuwa kama itatokea kila studio itatoa hit song italeta maana ya ushindani.

“Ushindani ni kila mtu kufanya kitu kizuri alafu yaani vinachuana leo hii kesho hii huo ndo ushindani”  Amesema Mr. T Touch.

Comments

comments

You may also like ...