Header

Aika adai Wasafi.com iliirudisha album yao ‘AIM’ kwenye chati

Msanii wa muziki wa Bongo Flava kutokea kundi la Navy Kenzo, Aika, amezungumzia kuhusu matokeo waliyoyapata baada ya kupeleka album yao, Above In A Minute wasafi.com.

Aika amesema,” Kwanza wasafi.com ni kama platform nyingine ambayo sisi Navy Kenzo tumeweka album yetu kama zinavyowekwa sehemu nyingine. Ila wasafi.com imekua platform ya kwanza East Africa kuipa nyimbo zetu ambazo mtu yoyote anaweza akadowndoad. Kwahiyo hatukuwapa mdundo hatukuwapa mkito, tuliwapa wasafi.com.

Aidha aliongeza na kusema, “Wasafi.com imetusaidia kwa kiasi kikubwa kurudisha album juu tena. Wengine walikuwa hawajui kama album imetoka kwa sababu Diamond pia ana nguvu na amekuwa akiitangaza wasafi.com, kwahiyo imekuwa na faida kubwa kutoka upande wetu. Na vilevile nahisi kila kitu kipo sawa kwasababu kuna watu wamekuWa wakinitumia screen shot na kunituma. Nyimbo zimekuwa on top kwa muda mrefu, kwahiyo inamaanisha kwamba iko vizuri.”

Above In A Minute ilitoka December mwaka jana.

Comments

comments

You may also like ...