Header

Ben Pol agoma kuomba msamaha kwa waliokwazwa na picha zake

Msanii wa muziki wa RnB kutoka Tanzania na hitmaker wa ngoma ‘Phone’ aliyomshirikisha Mr Eazi, Ben Pol ametoa sababu za kwanini hataomba msamaha kwa kile kinachohusisha picha zake zilizotafsiriwa kama picha za nusu utupu alizopost katika mtandao hata kusambaa kwa kasi zaidi katika mitandao ya kijamii.

Akizungumzia hicho kinachoendelea katika mitandao ya kijamii kama maoni na mitazamo tofauti kuhusu picha hizo, Ben Pol amesema kuwa hataomba msamaha na kuahidi kusimama na maana yake ya kuwa alichokifanya ni sanaa na si vinginevyo hata kuwasahi mashabiki wenye mtazamo tofauti na alichokilenga kutafuta maana halisi ya sanaa.

“mimi ninachowaambia ni kwamba watafute maana halisi ya sanaa, neno sanaa…unajua unaweza kuwa una-support kitu haukijui hauwezi kukielezea haujui maaana yake…maana ya sanaa, maana ya msanii nimeshangaa kuna watu wakubwa hawajui maana ya sanaa….” Alisem Ben Pol kupitia Ayo Tv.

Vil vile, Ben amebaisha kuwa lenog kubwa la kinachongojewa na wengi ni kuwasilisha maana ya wimbo wake ambao unataitwa ‘3’, wimbo ambao ameutaja kuwa na maudhui ya utekaji hivyo mashabiki wangoje kwakuwa ameshirikiana na Darassa na wako katika mikakati ya mwisho ya kushoot video karibuni video ambayo itafanyika Tanznaia.

Hata hivyo Ben Pol amesema kuwa kama shabiki ana uwezo wa kuhoji linapotokea jambo la namna yake na kutaka apate majibu basi iwe sawa sawa pia kwa mashabiki wasishangae msanii atakapowahoji kama biashara ya msanii husika inaposhuka kwa upande wa kukosa msaada wao wawe tayari kurekebisha ili muziki upate kusonga mbele.

 

Comments

comments

You may also like ...