Header

Bondia zao la Floyd Mayweather ashinda utetezi wa taji

Bondia machachari anayefuata nyayo za aliyekuwa bingwa wa dunia katika uzani wa middleweight Floyd Mayweather, Gervonta Davis ametetea taji lake la uzani wa Super Featherweight kwa kumuangusha Muingereza Liam Walsh katika raundi ya tatu ya pigano hilo lililoandaliwa katika ukumbi wa Copper Box Arena.

Katika mchezo huo uliowaktanaisha wakali hao baada ya raundi mbili za tahadhari Davis alimrushia makonde mazito mpinzani wake yaliomuangusha huku Walsh akiinuka lakini konde jingine la mkono wa kushoto kutoka kwa Davis lilimlazimu kiasi cha refa Michael Alexander kuingilia kati na kusimamisha pambano hilo.

Hata hivyo bondia Davis ambaye anakuzwa na Floyd Mayweather sasa hajashindwa katika mechi 18 na hivi majuzi alimshinda kwa njia ya knockout bingwa katika uzani huo ‘Jose Pedraza’.

 

 

 

 

Chanzo: BBC

Comments

comments

You may also like ...