Header

Diamond adai hana ugomvi na wamiliki wa mitandao mingine inayouza muziki Bongo

Tangu Wasafi.com mtandao wa kuuza nyimbo unaomilikiwa na Diamond uzinduliwe na baadhi ya wasanii kupeleka nyimbo zao kule, zipo stori za mtaani na minong’ono zinadai kuwa kama Diamond hayupo poa na baadhi ya wamiliki wa mitandao mingine ya kuuza nyimbo mtandaoni.

Ameamulia kulitolea ufafanuzi suala hilo kupitia kipindi cha XXL, Clouds FM.

“Sijawahi kuwa na vita na mtandao wowote wa kuuza nyimbo kwasababu kama wasafidotcom imekaa pale kwa nia njema tu. Tumeweka wasafidotcom kwasababu mitandao mingi inatoa nyimbo for free halafu wana download na kulipa kwenye mtandao lakini sisi ni tofauti, system ya kudownload iko tofauti kulipa wasanii, wasanii kupokea malipo yao na lengo ni kukuza industry.”

Ameongeza, Wasanii wanatakiwa kuwa na platform tofauti tofauti, sasa useme iwepo tu iTunes, lazima tukubaliane mianya tofauti tofauti ambayo kila msanii aone anapata kipato,” ameongeza.

BY SASHA NKYA

Comments

comments

You may also like ...