Header

Vanessa Mdee aliongozana na staa huyu wa Marekani kwenye tuzo za Billboard

Tuzo za muziki za Billboard mwaka huu zimekiki zaidi pengine kuliko miaka mingi ya hivi karibuni. Pengine ni kutokana na rapper Drake mwenye mashabiki kibao kuvunja rekodi kwa kushinda tuzo 13 kwenye usiku huo wa Jumapili.

Hata hivyo, si mastaa wa Marekani tu ndio walihudhuria tuzo hizo, Tanzania ilikuwa na mwakilishi pia – Vanessa Mdee. Hitmaker huyo wa Cash Madame, aliongozana na supastaa Dj wa Marekani, Diplo wa kundi la Major Lazer.

Kwenye video aliyoiweka Instagram akiwa na staa huyo, Vanessa ameandoka, “Reunited with my Ric Flair @diplo
Wait for that Major Lazer x VeeMoney 🇹🇿 x 🇺🇸#billboardmusicawards.”

Diplo na kundi lake wamemshirikisha Vee Money kwenye wimbo unaotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Comments

comments

You may also like ...