Header

Rick Ross atoboa siri ya jina la Album ya Meek Mill

Rapa na mmiliki wa lebo ya MMG, Rick Ross jana aliamua kuongea na mashabiki na wafuasi kupitia akaunti yake ya Snapchat, akiwa mubashara Rick Ross alifichua jina la studio album ya tatu ya rapa Meek Mill.

Rick Ross alipozama katika mtandao wa SnapChat kwa video video ambayo pia ilikuwa live katika mtandao wa Youtube alionesha kuwa na taarifa njema kuhusu project kubwa ya Mieek Mill na kutaja kuwa album hiyo inakwenda kwa jina ‘Wins and Losses’ ambapo Meek Mill miezi kadhaa iliyopita alishatangaza kuwa muda wowote maxtape yake iliyopewa jina la ‘Dreamchaser 4.5’ itadondoka ahadi ambayo mashabiki mpaka leo wanaingoja.

“Ndo maana nalipenda jina la album mpya ya Meek Mill, ‘Wins and Losses’…ndo maana na nawaambia mhakikishe mnaipata hii. Baada ya hapa nenda katazame ukatazame movie…pata pesa, pata pesa kisha ukimbie. Wajali watu wako wewe” Alisikika Rick Ross katika video hiyo.

Hata hivyo rapa Meek Mill amekuwa mgumu hasa kipindi cha majuzi kati kwakuwa kimya kwa muda. Mapema mwezi huu Meek aliachia EP yenye ngoma tatu inayokwenda kwa jina ‘Meekend Music’ iliyoachiwa katika kusherehekea siku ya kutimiza umri wa miaka 30 ya kuzaliwa kwake.

Comments

comments

You may also like ...