Header

Mark Zuckerberg apata shahada Harvard, miaka 12 baada ya kuacha na kuanzisha Facebook

Miaka 12 iliyopita, Mark Zuckerberg aliacha chuo na kwenda kuanzisha mtandao wa Facebook. Pengine huo ulikuwa ni uamuzi muhimu zaidi katika maisha yake, kwakuwa Facebook imegeuka kuwa kampuni kubwa duniani na inayomiliki mitandao mingine ikiwemo Instagram na WhatsApp huku utajiri wake sasa ukifikia dola bilioni 61.9.

Na sasa ameipata shahada yake, asante kwa heshima aliyopewa na chuo hicho maarufu duniani. Akizungumza na wahitimu wengine wa chuo hicho Alhamis hii, Zuckerberg alitania kwa kusema, “If I get through this speech today, it’ll be the first time I actually finish something here at Harvard.”

Zuckerberg, alianzisha Facebook kwenye bweni lake mwaka 2004. Kitu ambacho kilianza kama mtandao wa kuwaunganisha wanafunzi wa Harvard, kiligeuka kuwa mtandao wenye watumiaji zaidi ya bilioni 2 sasa duniani.

Zuckerberg amfuatia bilionea mwingine aliyeacha chuo Harvard, Bill Gates, aliyezungumza na wahitimu wa chuo hicho miaka 10 iliyopita. Pamoja na kuanzisha Facebook, Zuckerberg pia alikutana na mke wake Priscilla Chan katika chuo hicho ambapo yeye alienda kuwa daktari wa watoto.

Comments

comments

You may also like ...