Header

Otile Brown ashauriwa na Mwanasheria wake juu ya kuishitaki Dreamland Music

Muimbaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya na hitmaker wa ngoma ‘Niseme Nawe’ aliyomshirikisha Barakah The Prince ‘Otile Brown’, ametoa sababu za kwanini hakuifungulia mashtaka record lebo ya Dreamland Music inayomilikiwa na Dr. Eddie ambayo ilitangaza kuwa hana haki ya kutumia nyimbo zote alizofanya chini yao.

Akizungumza na Dizzim Online Otile amesema kuwa alibadilisha maamuzi ya kufungulia mashitaka lebo hiyo mara baada ya kushauriana na mwanasheria wake mpaka kukubaliana kuwa hakuna sababu za kusumbuana na kutaja kuwa kama wangefanya hivyo wangepeoteza muda mwingi muda ambao wameamua kushiriki mambo mengine yenye tija.

“Kuhusu kushtaki Lebo ambayo nilikuwa chini yao mwaka jana nilibadilisha mawazo na kisa mimi nilitaka kuwafungulia mshatka sio kisa Youtube chanel kisa ni yeye kuandika kwamba siwezi kuperfom nyimbo zangu…” Alisema. Baada ya kumshirikisha Lawyer wangu, aliniambia kuwa haina maana kabisa…mwisho wa siku niliona sio jambo zuri nikapotezea na nikaona haina maana yoyote” Aliongeza Otile Brown.

Vile vile, Otile amesema kuwa ameamua kwasasa kufanya kazi mwenyewe bila manejimenti mapaka pindi atakapokutana na wadau wa muziki wanaojihusisha na kumeneji wasanii wenye vigezo anavyovihitaji katika muziki wake.

Hata hivyo Otile Brown baada ya ngoma ya ‘Yule mbaya’ ameachia kazi yake nyingine mpya inayokwenda kwa jina ‘Kistaarabu’ ngoma ambayo imeandaliwa na Teddy B na video kuongozwa na ‘X Antonio’

 

Comments

comments

You may also like ...