Header

Zabaleta akubali kujiunga na West Ham

Beki wa kulia wa klabu ya soka ya Manchester City Pablo Zabaleta, amekubali kujiunga na Klabu ya soka ya West Ham United pindi mkataba wakeutakapomalizika mwishoni mwezi Julai.

Zabaleta,32 atasaini mkataba wa miaka miwili na Klabu ya West Ham na kuanza rasmi kuitumikia miamba hiyo kutoka jijini London msimu ujao, baada ya kuitumikia Manchester city miaka 9 tangu alipojiunga nayo mwaka 2008 akitokea katika klabu ya Espanyol ya nchini Hispania.

Mpaka sasa beki huyo mwenye asili ya Argentina amecheza michezo zaidi ya 300 katika klabu ya Manchester City huku akifunga jumla ya magoli 11 katika mashindano yote na kuisaidia City kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza mara mbili msimu wa 2011/2012 na 2013/2014 pamoja na kombe la Ligi maarufu kama FA Cup mwaka 2010/2011.

Tangu kocha mkuu wa klabu hiyo Slaven Bilic kuanza kuinoa klabu hiyo mwaka 2015, Usajili wa Pablo Zabaleta unakuwa ni usajili wa kwanza mkubwa kufanyika katika klabu hiyo ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Comments

comments

You may also like ...