Header

Arsenal kuwakosa Gabriel na Koscielny fainali FA

Klabu ya soka ya Arsenal itawakosa mabeki wake Laurent Koscienly pamoja na Gabriel Paulista katika mchezo wa leo wa fainali ya FA Cup dhidi ya Chelsea, mchezo utakaopigwa katika dimba la Wembley nchini Uingereza.

Koscienly anatumikia kadi nyekundu aliyopata katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu dhidi ya Everton pamoja na Gabriel Paulista ambae aliumia katika mchezo huo pia atakua nje kwa zaidi ya wiki sita huku kukiwa na hati hati kuwakosa nyota wengine akiwemo Alex Oxlade-Chamberlain aliyeanza mazoezi hivi karibuni baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Southampton pamoja na Shkodran Mustafi ambae hajafanya mazoezi na kikosi hicho tangu kumalizika kwa ligi kuu.

Kwa upande wa wapinzani wao Chelsea ambao ni mabingwa wa Ligi kuu nchini Uingereza msimu huu, kikosi chao hakina majeruhi yoyote kuelekea mchezo huo utakaopigwa majira ya saa moja na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Mchezo wa leo ni muhimu kwa Arsene Wenger kupata matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kukinoa kikosi hicho cha ‘The Gunners’ msimu ujao kufuatia mashabiki wa Arsenal kutaka aondoke huku mkataba wake ukiwa umesalia miezi miwili kumalizika.

Comments

comments

You may also like ...