Header

Moni Central ashindwa kusikiliza ushari wa familia yake kuhusu muziki

Rapa na mkali wa ngoma ya ‘Sembe Dona’ na ‘Usimsahau Mchizi’ aliyomshirikishwa na Roma ‘Moni Central Zone ameshindwa kusikiliza kauli ya Shangazi yake aliyemtaka asijihusishe tena na muziki kauli iliyoitoka katika kipindi ambacho Moni aliingia katika tukio la utekwaji tukio lililomhusisha Roma na wenzake.

Akipiga stori na Dizzim Online Moni amesema kuwa ni kweli tangu ameanza muziki hajawahi kupewa ruhusa na wakubwa wa familia kwa kuwa waliamini anaweza kufanikiwa zaidi kama atatumia elimu atakayo ipata tofauti na atakapofanya muziki. Moni ameendelea na muziki bila kujali changamoto ya shangazi yake kwa lengo la kuwahakikishia kuwa anaweza kufanikia katika kitu ambacho anakipenda.

 

“kwanza sijaaga wala sijaomba ruhusa ya kuachia nyimbo nyingine, unajua hili suala ni gumu saa kwenye fmamilia na yule ni shangazi yangu ambaye ana uvhungu sana na mimi na mkali sana. Sikuwahi kupata ruhusa kwasababu walikuwa hawana imani wanaamini ntafanikiwa zaidi na shule”

Amesema Moni.

 Mimi nimejaribu kumuonesha kwamba hatua zangu nitakazopiga ili kumtoa ile imanai yake kwamba anaona sitafanikiwa…kwa ndo maana unaona nimejitoa kimaso maso kwenda kufanya kazi ili ni prove wrong nimuoneshe kuwa hii ni kazi ambayo niliyoichagua na inaweza kunisaidia kwenye maisha yangu licha ya kwamba nina elimu”

Amesema Moni.

Vile vile Moni amebainisha kuwa katika safari yake ya kufanya muziki hakuaga kwakuwa tafsiri ya muziki kwa wanafamilian wake sio rahisi kuruhusiwa afanya muziki na kusema kuwa mtazamo wao ni wayaone mafanikio ambayo wanayatamani jambo ambalo kwake amonesha kuwa na imani ya kifanikiwa kimuziki kulingana na muda unavyozidi kwenda.

Hata hivyo Moni amewaomba mashabiki waendelee kumsupport katika muziki wake huku akiwataka wawe tayari kupokea video ya wimbo wake mpya wa ‘Tuaishi nao’ itaakayo achiwa wiki ijayo.

 

 

Comments

comments

You may also like ...