Header

Diamond Platnumz athibitisha utayari wa kufanya kolabo na Ali kiba kuwa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz ameweka wazi kuwezekano wa kufanya kolabo na Ali kiba.

Akiongea na NTV Kenya Diamond amesema kuwa alisha kutana na Ali Kiba katika wimbo wa pamoja kwenye project ya Kigoma All Stars na kuhaidi kuwa wawili hao wanaweza kushirikiana kwa nia ya kufanya muziki mzuri na kuitangaza Tanzania.

“Mimi na Ali Kiba ni watanzania ambao ni wanamuziki na tunashukuru kuona tunapendwa wote Kenya kwasababu ni furaha yetu” Aliendelea, alipoulizwa kama kuna siku watafanya Kolabo, “of Corse, tushafanya tulifanya nyimbo moja ya Kigoma All Stars na nafikiri tutafanya pia kwasababu ni jambo zuri.

Na nimefurahi sana kuona kama tunapata support kubwa sana kutoka Kenya kwasababu mimi naonaga Kenya ni kama nyumbani so kuona pia tunapendwa sisi tunashukuru sana na tunawahaidi kwamba hatutawaangusha kila nyimbo zitakazo toka zitakuwa nzuri na mtazipenda” Alisema Diamond Platnumz.

Hata hivyo Diamond ameongeza anategemewa kuachia album yake itakayokwenda kwa jina ‘Nothing But Bongo Flava’ ambayo inatajwa kuwa la ngoma za bongo fleva pekee.

Comments

comments

You may also like ...