Header

Inakumbukwa siku kuzaliwa kwa Rais wa Marekani aliyeuwawa kwa kupigwa risasi

Leo ni siku ya mfanano wa kuzaliwa kwa Rais wa 35 wa Marekani John Fitzgerald Kennedy au John F. Kennedy Rais aliyeuwawa kwa kupigwa risasi.

Mnamo mwaka 1960 alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani na kihistoria anatajwa kuwa ni Rais pekee muumini wa Kanisa Katoliki katika historia ya nchi ya Marekani.

John F. Kennedy

Tukio la kupigwa risasi kwa Rais Kennedy lilitokea tarehe 22 Novemba 1963 ambapo inahesabika kuwa alikaa madarakani kwa muda wa miaka 2 na Miezi 10 na siku kadha ambapo aliacha mke na watoto wawili.

Aliuawa mjini Dallas Texas, ambapo anatajwa kuwa Rais aliyeingia kwenye madaraka akiwa mdogo pia Rais aliyefariki katika umri mdogo ambapo alifariki akiwa ni mwenye umri wa miaka 46.

Comments

comments

You may also like ...