Header

Kerber atupwa nje mashindano ya French Open

Mchezaji nambari moja kwa ubora katika mchezo wa Tenesi kwa upande wa wanawake Angelique Kerber ameondolewa katika raaundi ya kwanza ya mashindano ya French Open yanayoendelea mjini Paris nchini Ufaransa.
Mshindi huyo mara mbili wa ubingwa wa Grand Slam, amepoteza mchezo dhidi ya Mrusi Ekaterina Makarova kwa jumla ya seti 6-2 6-2 ndani ya saa 1 na dakika 22 na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza anaeshikilia nafasi za juu kuondolewa katika mashindano hayo kwenye mzunguko wa kwanza.
Makarova, 28 anaeshikilia nafasi ya 40 kwa ubora katika viwango vya Tenesi kwa upande wa wanawake atakutana na mchezaji Lesia Tsurenko kutoka Ukraine katika mzunguko wa pili baada ya Tsurenko kushinda hapo jana dhidi ya Kateryna Kozlova.
Keber mwenye asili ya Ujerumani amekua akipambana kurejea katika kiwango chake tangu mwaka 2017 kuanza, amefanikiwa kuingia fainali moja na kushinda michezo mitatu tu katika katika mashindano tofauti ya kimataifa.
Mashindano hayo ya French Open yameanza kutimua vumbi hapo jana Mei 28 na yatafikia tamati Juni 11 katika mji wa Paris nchini Ufaransa. Bingwa mtetezi katika mashindano haya kwa upande wa wanawake ni Muhispania Garbiñe Muguruza kutoka Hispania aliyenyakua taji hilo mwaka Jana kwa kumfunga Serena Williams aliyekuwa akishikilia nafasi ya kwanza kwa ubora.

Comments

comments

You may also like ...