Header

Man City kuvunja rekodi kwa Golikipa wa Benfica

Klabu ya Manchester city ipo tayari kuvunja rekodi ya dunia kwa upande wa Golikipa kwa kuripotiwa kutaka kumsajili mlinda mlango wa Benfica Ederson Moraes kwa kitita kinachokadiriwa kuwa Paundi milioni 45.
Mlinda mlango huyo,23 amekuwa akiwindwa na Pep Gudiola ambae ni kocha mkuu wa Manchester City tangu msimu uliopita wakati kocha huyo alipojiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Buyern Munich ya nchini Ujerumani.


Edson mwenye asili ya Brazili amekaririwa akisema kuwa mchezo wa fainali dhidi ya Vitoria Guimaraes siku ya Jumapili unaweza kuwa mchezo wake wa mwisho klabuni hapo, hali inayoashiria mchezaji huyo kuelekea Etihad.
“Bado sijui chochote, ila nadhani hii inaweza kuwa mechi yangu ya Mwisho na Benfica”. Alisema mlinda mlango huyo alipohojiwa na Gazeti la nchini Ureno linalofahamika kama ‘Record Newspaper’.
Edson Moraes alijiunga na Benfica mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 16, amewai vitumikia vilabu vya Ribeirao na Rio Ave vyote vya nchini Ureno na baadae kujiunga tena na Benfica mwaka 2015.


Kama Man City watafanikiwa kumsajili mlinda mlango huyo kwa ada ya pauni milioni 45, Edson Moraes atavunja rekodi ya Dunia kwa upande wa walinda Mlango ambayo inashikiliwa na Gianluigi Buffon aliponunuliwa na Juventus akitokea klabu ya Parma mwaka 2001 kwa ada ya shilingi Paundi milioni 32.6.

Comments

comments

You may also like ...